Kwa shule za msingi na sekondari Tanzania

Achana na Excel na kujaza matokeo kwa mikono!

Pakia alama za wanafunzi, mfumo utakokotoa jumla, wastani, madaraja na nafasi wenyewe. Tengeneza ripoti, andaa ratiba, na tuma matokeo kwa wazazi kwa SMS — yote mahali pamoja.

Mtihani wa Nusu Muhula
RIPOTI YA MWANAFUNZI
SOMOALAMADARAJA
KISWAHILI90A
ENGLISH60C
BIOLOGY87A
CHEMISTRY95A
MATH45D
WASTANI75.4A

Sifa Kuu

Kila kitu unachohitaji kuandaa matokeo — mahali pamoja.

Uchambuzi wa Matokeo

Jumla, wastani, daraja na nafasi hukokotolewa kiotomatiki — kwa kila somo na kwa jumla. Takwimu za ufaulu wa darasa na kumi bora.

Ripoti Tayari Kuchapisha

Kadi ya matokeo ya kila mwanafunzi kwa muundo wa TAMISEMI — tayari kuchapisha au kuhifadhi PDF. Pia unaweza kupakua jedwali kwa Excel (CSV).

Arifa za SMS kwa Wazazi

Tuma muhtasari wa matokeo kwa wazazi wote kwa mpigo mmoja, ukitumia namba za simu zilizoingizwa. Gharama zinaonyeshwa kabla ya kutuma.

Portal ya Wazazi

Mzazi anaangalia matokeo ya mwanae kwa simu, kwa namba ya siri — bila kufungua akaunti. Shule inaamua ni matokeo yapi yaonekane.

Ratiba ya Vipindi

Weka mgao wa walimu na masomo, kisha mfumo unaandaa ratiba ya wiki nzima wenyewe — ukikwepa migongano ya walimu.

Ufuatiliaji wa Mahudhurio

Weka mahudhurio ya kila siku (Yupo, Hayupo, Amechelewa, Ruhusa) na uone muhtasari wa kila mwanafunzi na asilimia ya mahudhurio.

Kuingiza Wanafunzi kwa Excel

Pakua template ya Excel, jaza majina, kisha uipandishe. Au bandika orodha yako — mfumo unatambua safu za majina wenyewe.

Walimu na Watumiaji

Mmiliki huongeza walimu na watumiaji wa mfumo, huwapa majukumu (mmiliki, taaluma, mwalimu), na hutumia namba ya mwaliko kuwaunganisha.

Data Salama na Imetengwa

Kila shule inaona data yake pekee — kizuizi kiko ndani ya database yenyewe. Data yako haifikiki na shule nyingine yoyote.

Bei

Kifurushi kimoja kwa shule nzima kwa muhula — bila kujali idadi kubwa ya walimu.

NDOGO

Hadi wanafunzi 300

TZS20,000/muhula
  • Uchambuzi wa matokeo & ripoti
  • Mahudhurio & ratiba ya vipindi
  • Portal ya wazazi
  • Watumiaji hadi 5
Anza sasa
Maarufu zaidi

KATI

Wanafunzi 301 – 800

TZS35,000/muhula
  • Yote ya kifurushi cha NDOGO
  • Kuunganishwa na mtoa huduma wa SMS (shule hulipia SMS)
  • Watumiaji hadi 15
  • Msaada kwa simu
Anza sasa

KUBWA

Wanafunzi 800+

TZS50,000/muhula
  • Yote ya kifurushi cha KATI
  • Watumiaji bila kikomo
  • Msaada wa kipaumbele
  • Mafunzo kwa walimu
Anza sasa

Muhula wa kwanza ni bure kujaribu. Malipo hufanyika baada ya kuridhika.

Jinsi ya Kulipia

Jaribu bure, kisha lipia kwa benki ili kuendelea. Hakuna malipo ya awali.

  1. 1

    Sajili bure

    Fungua akaunti na usajili shule yako bila malipo yoyote.

  2. 2

    Tumia muhula wa kwanza

    Jaribu vipengele vyote — matokeo, ripoti, ratiba, mahudhurio.

  3. 3

    Lipa kwa benki

    Ukiridhika, lipa ada ya kifurushi chako kwa akaunti ya benki iliyo pembeni.

  4. 4

    Tuma risiti

    Tuma picha ya risiti kwa WhatsApp/simu (+255 765 065 063), huduma yako itaendelezwa.

Lipa kwa akaunti ya benki

NMB BANKBenki
Jina la akauntiMUKENDI STATIONERIES AND GENERAL SUPPLYNamba ya akaunti50910038654

Baada ya kulipa, tuma picha ya risiti kwa +255 765 065 063 ukitaja jina la shule yako.

Mfumo huu ni kwa ajili ya nani?

Shule

  • Simamia wanafunzi, walimu na masomo
  • Jaza alama na toa ripoti za matokeo
  • Andaa ratiba ya vipindi kiotomatiki
  • Tuma matokeo kwa wazazi kwa SMS

Walimu wa Taaluma

  • Uchambuzi wa ufaulu kwa darasa na somo
  • Panga mgao wa walimu na vipindi
  • Fuatilia nani anajaza alama
  • Toa takwimu za kumi bora

Wazazi

  • Angalia matokeo ya mwanao kwa simu
  • Tumia namba ya siri — bila akaunti
  • Pokea matokeo kwa SMS
  • Chapisha au hifadhi ripoti (PDF)

Jinsi inavyofanya kazi

Hatua nne, dakika chache.

1

Sajili shule yako

Sajili shule na uwe mmiliki. Masomo na madaraja ya kawaida yamewekwa tayari.

2

Sajili wanafunzi

Ingiza wanafunzi mmoja mmoja, kwa template ya Excel, au kwa kubandika majina.

3

Jaza alama

Tengeneza mtihani, jaza alama — hesabu, madaraja na nafasi vinajipanga vyenyewe.

4

Toa ripoti & arifa

Chapisha ripoti, pakua Excel, au tuma matokeo kwa wazazi kwa SMS.

Anza leo — bila malipo

Sajili shule yako sasa, uwe mmiliki wa mfumo, na uache kujaza matokeo kwa mikono.